Raia saba wa Uturuki waachiwa huru nchini Libya na kurejeshwa nyumbani

 


Wizara ya mambo ya nje ya Uturuki imesema leo kuwa raia saba wa nchi hiyo waliokuwa wamezuiwa Mashariki mwa Libya wamerejeshwa salama nchini humo.


Shirika la habari linalomilikiwa na serikali Anadoli limeripoti kuwa watu hao ambao wengi walikuwa wafanyakazi wa migahawa walikuwa wamezuiwa katika eneo hilo la Mashariki la Libya kwa miaka miwili. 


Shirika la Anadolu limeendelea kuripoti kuwa idara ya ujasusi ya Qatari ilishirikiana na idara ya kitaifa ya ujasusi nchini Uturuki MIT katika juhudi za kutafuta kuachiliwa huru kwa njia salama raia hao saba wa Uturuki. 


Katika taarifa, wizara ya mambo ya nje ya Uturuki ilizishukuru serikali za Qatar na Libya hasa idara husika zilizochangia katika mchakato wa kuachiliwa kwa watu hao. 


Uturuki ilituma wanajeshi wake nchini Libya chini ya makubaliano ya mwaka 2019 kuhusu ushirikiano wa kijeshi uliotiwa saini na serikali ya Maridhiano ya Kitaifa GNA, kuisaidia kukabiliana na mashambulizi ya vikosi vya kamanda mwenye nguvu nchini humo Khalifa Haftar vilivyoko mashariki mwa Libya.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia