Raia watano wa China watekwa nyara DRC


Washambuliaji waliokuwa na silaha wamemuuwa afisa mmoja wa polisi na kuwateka nyara raia watano wa China usiku wa kuamkia leo karibu na mgodi mmoja Kusini Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo. 


Haya yamesemwa leo na afisa mmoja na msemaji wa jeshi katika eneo hilo Meja Dieudonne Kasereka.Meja Kasereka amesema kuwa kundi hilo la washambuliaji walikabiliana na polisi kwa kufyetuliana risasi. 


Haikubainishwa wazi aliyehusika na shambulizi hilo karibu na kijiji cha Mukera Katika mkoa wa Kivu Kusini mwa nchi hiyo. 


Tayari kuna mvutano katika uhusiano kati ya makampuni ya uchimbaji madini ya China na mamlaka ya eneo hilo inayosema kuwa baadhi ya makampuni yanafanya kazi kinyume cha sheria bila leseni. Hata hivyo msemaji wa ubalozi wa China nchini humo hakujibu ombi la tamko kuhusu tukio hilo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia