Ufahamu Msikiti wa Mali unaokarabatiwa kila mwaka

 Msikiti Mkuu wa Djenné katika jangwa kame la kusini mwa Mali, umejengwa ni jengo linalovutia macho.


Msikiti huu wenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 91 nchini Mali, ndio jengo refu zaidi la udongo kujengwa duniani.


Muundo wake ni mojawapo ya mijengo maarufu zaidi katika eneo la Sahil.


Msikiti wa Gargantuan bila shaka ndio kitovu cha maisha katika jiji hilo.


Watoto hutumia sehemu ya Msikiti huo kujifunza Qoran.


Msikiti huo uliopo kati kati ya Mito Niger na Bani huko Djenné umedumu takriban miaka 250, zinazoifanya kuwa wa zamani zaidi katika miji ya jangwa Sahara barani Afrika.

Ulijengwa kati ya karne ya 13 na 18 kama kituo kikubwa cha usafirishaji wa bidhaa kama vile chumvi na dhahabu.

Watu waliopitia kituo hicho walinunua vitabu vya kidini kwa kuwa Uislamu ulikuwa umesambaa kote katika eneo hilo.

Haikuchukua muda mrefu kwa Djenné kuwa kituo cha masomo ya Kiislamu, na ujenzi wa Msikiti Mkuu hatimaye ulifanyika mnamo 1907.

Ushawishi wa Uislamu unadhihirika leo, huku wanafunzi mara nyingi huonekana wakijifunza Quran katika mitaa ya Djenné.


Msikiti huu mkubwa una minara mitatu tofauta, na mamia ya miti iliyokatwa kutoka kwenye mtende, inayojulikana kama 'toron', ambayo inaonekana kwenye kuta za jengo hilo.

Una baridi hata siku za joto kali. Wavu wenye nguzo 90 za mbao iliyowekwa upande wa ndani kuzuilia paa na kuta, huilinda dhidi ya jua.

Paa, kwa upande mwingine, ina nafasi kadhaa ambazo hufanya iwe rahisi kwa hewa safi kuingia msikitini wakati wa majira ya joto, lakini wakati wa msimu wa mvua nyasi nyingi huondolewa.

Mskiti huo unaweza kusaliwa na hadi watu 3,000.


Kuta za Msikiti huo mkubwa mjin Djenné hujengwa upya mwezi Aprili kila mwaka, siku moja ikitengwa kwa shughuli hiyo inayofahamika kama Crépissage.

Muundo wa msikiti unahitaji kuimarishwa kila mwaka- pamoja na nyumba za udongo maarufu za jiji - kabla ya msimu mfupi wa mvua nchini Mali, ambayo hunyesha miezi ya Julai na Agosti. Mvua msimu huo ni kubwa.


Mradi huu mkubwa unahakikisha kuwa msikiti unahimili msimu wa mvua, ingawa muundo wake hubadilika kila mwaka.

Udongo sio tu kipengele muhimu cha kutengeneza kilichoundwa ili kuzuia kuta za msikiti kutokana na kupasuka na kuanguka, lakini pia ni sherehe ya jamii ya Djenné, kwa mujibu wa historia yao na utamaduni na imani za jadi.

Kabla ya kujengwa msikiti huo, watu wa mji huo walikuwa wakiamka usiku huo huku baadhi yao wakisherehekea huku wengine wakiabudu na kuswali zaidi. Saa 4:00 asubuhi, ni alama ya mwanzo wa moja ya siku nzuri zaidi katika historia ya Djenne.

Kabla ya kujengwa msikiti huo, watu wa mji huo walikuwa wakiamka usiku huo wakati yao wakisherehekea, wengine wakiabudu na kuswali zaidi. Saa kumi alfajiri, ni ishara ya mwanzo wa moja ya siku nzuri zaidi katika historia ya Djenne.

Wakati wa ukarabati, kila timu kutoka kila kitongoji cha Djenné hushindana ili kukarabati msikiti, kutekeleza kazi hiyo kwa uangalifu na kwa usahihi.





Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia