Shirika la Upelelezi la Urusi - SVR limepuuzulia mbali madai yanayoongezeka ya nchi za Magharibi kuwa Moscow inapanga kuivamia Ukraine.
Katika taarifa ya nadra kwa vyombo vya habari, Shirika la SVR imesema limesema Wamarekani wanatoa taswira ya kutisha ya msafara wa vifaru vya Urusi ambavyo vitaanza kuiponda miji ya Ukraine, wakisema wana habari za kuaminika za nia kama hizo kutoka kwa Urusi.
Urusi inasema Marekani inatuma kwa washirika wake habari za uwongo kabisa juu ya mkusanyiko wa vikosi kwenye mipaka ya nchi yake kwa ajili ya uvamizi wa kijeshi nchini Ukraine.
Nchi za Magharibi mwezi huu zimezua wasiwasi kuhusu shughuli za jeshi la Urusi karibu na Ukraine, huku Marekani ikisema ina wasiwasi wa kweli juu ya kile ilichoita "shughuli zisizo za kawaida."