Akizungumza katika mkutano wa video na wakuu wa nchi na serikali za ASEAN, Rais Xi amesema China pia itatoa msaada wa dozi milioni 150 za chanjo ya Covid-19. Amesema China hailengi kutumia ubabe wa kisiasa, licha ya vitendo vya jeshi lake la wanamaji katika Bahari ya Kusini mwa China, ambako ina mizozo kadhaa ya mipaka na majirani zake.
Xi amesema China inataka kuishi kwa amani na majirani zake na kufanya kazi pamoja ili kuwa na amani ya kudumu katika kanda hiyo.
Katika siku za karibuni, kumekuwa na matukio mapya ya wanachama wa ASEAN Ufilipino, Malaysia na Vietnam katika maeneo ya ndani na karibu na bahari ya Kusini mwa China ambayo China inadai kuwa ni mipaka yake.