Waumini wa kanisa katoliki nchini waombwa kuonesha karama walizopewa na Mungu

 


Waumini wa kanisa katoliki nchini waombwa kuonesha karama walizopewa na Mungu.


Raisi wa Baraza la Maskofu katoliki Tanzania Mhashamu Gervas Nyaisonga amewataka waumini wa kanisa katoliki kuonesha karama walizopewa na Mungu ili kuliendeleza kanisa Hilo.


Mhashamu  Nyaisonga ambaye pia ni askofu wa Jimbo  katoliki la Mbeya amesema hayo Leo katika misa ya kutabaruku kanisa kuu katoliki kigoma na kuweka wakfu altare ya kanisa hilo.


Aidha amesema kuwa wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na Askofu wa Jimbo katoliki la Kigoma Mhashamu Joseph Mlola ambaye kwa kushirikiana na waumini jimboni humo wamefanikiwa kufanya maendeleo makubwa ikiwemo kukaravati kanisa kuu na maendeleo mengine mbalimbali kwa kushirikiana na wafadhiri mbalimbali.


Hata hivyo kwa upande wake Askofu wa Jimbo hilo Joseph Mlola amewashukuru waumini wake kwa majitoleo ya Hali na Mali katika kufanikisha ukaravati wa kanisa Hilo uliogharimu milioni miasaba na kuwasihi waendelee na moyo huo wa ushirikiano bila kuchoka.


Sanjari na hilo adhimisho na misa hiyo ya kutabaruku kanisa imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini,kisiasa pamoja na kiserikali.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi