Waziri wa Lebanon aonya juu ya athari ya mzozo wa kidiplomasia na Saudi Arabia


Waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon Bassam Mawlawi amesema kuchelewa kusuluhishwa kwa mzozo wa kidiplomasia na mataifa ya ghuba kunatishia kuiathiri nchi hiyo ambayo tayari inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi. 


Mawlawi amesema kusuluhishwa kwa mzozo huo wa kidiplomasia kunafaa kuanza kwa kujiuzulu kwa Waziri wa habari aliyekosoa uvamizi wa Saudi Arabia nchini Yemen. 


Saudi Arabia, ambayo ni mshirika wa karibu wa Lebanon ilimuita nyumbani balozi wake na kumtaka balozi wa Lebanon nchini humo kuondoka kufuatia kauli ya Waziri George Kordahi. 


Kordahi alisema vita vya Yemen havina maana yoyote na kuvitaja kuwa, ni uchokozi wa muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia. Hata hivyo, Kordahi amekataa kuomba msamaha au kujiuzulu licha ya shinikizo dhidi yake.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items