Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Aung San Suu Kyi apewa kifungo cha jela

 


Kongozi wa kiraia wa Myanmar aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi Jumatatu amepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha jela cha miaka minne kwa tuhuma za kuleta nchini vifaa vya mawasiliano kinyume cha sheria, pamoja na kukiuka kanuni za kujiepusha na maambukizi  ya corona. 


Vyanzo vyenye taarifa za kuaminika kutoka kwenye mahakama ya jiji kuu la Naypyitaw vimeambia vyombo vya habari kwamba Suu Kyi alihukumiwa kifungo cha miaka miwili kutokana na kukiuka sheria za uagizaji bidhaa nchini na kuleta vifaa vya mawasiliano vya walkie talkie, kinyume cha sheria, pamoja na kukiuka sheria za nchi za majanga ya kiasilia ambazo zinalinda dhidi ya maambukizi ya corona.


Hukumu ya Jumatatu imekuja, mwezi mmoja baada ya Suu Kyi kupatikana na hatia nyingine ya kuchochea umma. Iwapo Suu Kyi mwenye umri wa miaka 76 atapatikana na hatia kutokana na mashitaka yote yanayomkabili, basi huenda akapewa kifungo cha zaidi ya miaka 100 jela na utawala wa kijeshi uliomuondoa madarakani Februari mosi mwaka wa 2021. Suu Kyi pia anakabiliwa na tuhuma za kutoa siri za serikali, utumizi mbaya wa ardhi pamoja na kupokea fedha zisizo halali.

Post a Comment

0 Comments