Mbunge Kamonga atoa msaada kwa mchezaji anayekwenda kucheza soka la kulipwa Uturuki


Na Amiri Kilagalila,Njombe.

Mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph Kamonga amechangia fedha kiasi cha Milioni 1,000,000 ili kuweza kusaidia safari ya mchezaji wa Tembo Warriors Frank Ngairo mwenyeji wa wilaya ya Ludewa anayetarajia kwenda nchini Uturuki kucheza soka la kulipwa.

Kamonga ametoa mchango huo jijini Dar es Salaam mara baada ya kupata taarifa kuwa mchezaji huyo anakumbana na changamoto ya kukosa kiasi cha fedha kwaajili ya malipo ya Visa pamoja na tiketi.

Akimkabidhi kiasi hicho mbele ya viongozi wa Shirikisho la soka la watu wenye ulemavu Tanzania (TAFF) anasema kuwa licha ya kuwa mchezaji huyo anatokea Jimboni kwake bado yeye ni mdau mkubwa wa michezo nchini.

"Ngairo anakwenda kua mfano wa kuingwa miongoni mwa vijana walemavu nchini ambao Wana ndoto za kucheza soka la Mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu jambo ambalo wakazi wa Ludewa tutajivunia nalo" amesema Kamonga

"Mchango huu hautakua mchango wa mwisho kwani lazima nihakikishe kijana huyu anatimiza ndoto zake na pia ninawawakilisha wakazi wote wa Ludewa ambao Kama wangekua karibu basi nao wangetoa chochote kwaajili ya kijana wetu" aliongeza kusema Kamonga

"Hata hivyo mimi siyo wa kwanza kwani nakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan alimtaja mchezaji hivyo binafsi ninafarijika kuona pia ni miongoni mwa wachezaji walemavu wanaokwenda kuliinua soka la walemavu nchini."anasema Mbuge wa Rudewa Kamonga.

Ngairo amesema kuwa anamshukuru Mbunge huyo kwa kumshika mkono hivyo hatomsahau kwenye maisha yake ya soka.

"Hakika kupitia mchango huu nimeweza kuona kuwa watu wapo nyuma yangu kuhakikisha kuwa nasonga mbele bila kurudishwa nyuma na changamoto yoyote ile,"alisema Ngairo

"Pia shukrani zangu ziwaendee TAFF ambao wakua pamoja nami mwanzo mwisho kuhakikisha safari yangu inakamilika ya kwende kuiwakilisha nchini," anaendelea na kusema kuwa anawashukuru Watanzania wote wanaokwenda msapoti na pia wasiache kumsapoti

"Najua kuwa ninajukumu la kuonyesha kuwa Tanzania tuna vipaji vikubwa vya kucheza kandanda la watu wenye ulemavu hivyo lazima niwe Nuru kwa wachezaji wengine."anasema Ngairo

Naye Rais wa Shirikisho la soka kwa watu wenye ulemavu (TAFF), Peter Sarungi hakua nyuma kumpongeza Mbunge huyo kwa kujitolea kwa moyo wote kutatua changamoto iliokua ikiwakabili.

"Sisi Kama Shirikisho husika linalowatunza vijana Hawa wenye ulemavu tunakushuru kwa dhati kwa kuja na kutushika mkono na kuonyesha kuwa umeguswa na jitihada zetu za kuhakikisha mchezaji wetu anasafiri kwenda nchini Uturuki" anasema Sarungi.

Frank Ngairo anatarajiwa kwenda nchini Uturuki kujiunga na timu ya Izimir BBSK inayoshiriki ligi kuu ya walemavu nchini humo.

 

Post a Comment

0 Comments