Rais wa Syria Bashar al Assad amemtembelea mshirika wake wa karibu wa kikanda na kiongozi wa juu kabisa nchini Iran Ayatollah Khamenei hii leo, hii ikiwa ni kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya Iran.
Assad anayezuru Iran kwa mara ya pili tangu kuanza kwa vita ya Syria mwaka 2011, pia amekutana na rais wa Iran Ebrahm Raisi, limeripoti shirika la habari la Irani, IRNA.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amirabdollahian alisema wakati aakiwa ziarani mjini Damascus mwezi Machi kwamba kipaumbele cha Iran kilikuwa ni kuimarisha mahusiano na Syria katika kuubadilisha mtizamo wa kimataifa baada ya Urusi kuivamia Ukraine.
