Joe Biden alianguka wakati akishuka katika baiskeli Jumamosi Juni 18,2022 baada ya safari karibu na nyumbani kwake ufukweni katika jimbo la Delaware nchini humo.
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 79 alikuwa katika matembezi na mkewe Jill walipokuwa wakiadhimisha miaka 45 ya ndoa yao ambapo Biden alianguka alipokuwa akijaribu kushuka kwenye baiskeli yake ili kuwasalimu wafuasi wachache waliokuwa katika eneo hilo
Hata hivyo taarifa ya Ikulu ya Marekani ilisema Biden hakuumia ila mguu wake ulinasa kwenye sehemu ya kukanyagia wakati wa kuendesha baiskeli.
0 Comments