Na Cyprian Magupa, Mwanza.
Shirika la umeme Tanzani(TANESCO)Mkoa wa Mwanza limejipanga vyema kuhakikisha linawahudumia wateja wake katika maonyesho ya sikukuu ya wakulima maarufu kama (nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nyamuhongoro jijini hapa.
TANESCO inaendelea kuwakaribisha wananchi kufika katika banda lao ili kuendelea kujifunza kuhusu huduma na elimu mbalimbali zinazohusu Sekta ya nishati na Kilimo .
Kama kaulimbiu isemavyo,“KILIMO NI BIASHARA, SHIRIKI KUHESABIWA KWA MIPANGO BORA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI” TANESCO wameendelea kuuelimisha umma kuwa upatikanaji wa umeme unasaidia katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kwani umeme umeendelea kuongeza thamani ya bidhaa mbalimbali kama shughuli za usindikaji, uhifadhi wa vyakula kwa muda mrefu, kurahisisha utengenezaji wa vifungashio vya bidhaa na zaidi kabisa, nishati ya umeme ni rafiki kwa kilimo cha kisasa.
Aidha katika hatua nyingine TANESCO wamejipanga kuwaonyesha wateja wao video za maendeleo ya mradi mkubwa wa Bwawa la Mw.Julius Nyerere ambalo linatarajiwa kuzalisha umeme wa MW 2115 pindi litakapokamilika kwa asilimia 100%, ambapo Shirika linaahidi upatikanaji wa huduma bora na uhakika ya umeme mara baada ya mradi huo kukamilika na kuendelea kuongeza thamani katika sekta ya kilimo.
Kwa upande wake ofisa uhusiano huduma kwa wateja kutoka shirika hilo Mkoani Mwanza Bi.Flaviana Moshi ameendelea kuwakumbusha wateja wao kutumia huduma ya Ni-konekti app inayopatikana kwa simu janja na simu za kawaida.
Utumiaji wa huduma hiyo kunawarahisishia wateja wapya kupunguza msongamano wa gharama na muda pindi wanapohitaji huduma za kuunganishiwa umeme ,lakini pia faida nyingine za mfumo huo ni kurahisisha na kuondoa vishoka ambao waliku mtu kati katika utoaji wa huduma kwa wateja.


