Mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag anasema "haikubaliki" kwamba wachezaji kadhaa, akiwemo Cristiano Ronaldo, waliondoka kwenye mechi ya kirafiki Jumapili kwenye Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Rayo Vallecano mapema.
Ronaldo, katika mchezo wake wa kwanza wa kujiandaa na msimu mpya, alibadilishwa wakati wa mapumziko.
Alipigwa picha akiondoka na Diogo Dalot, ambaye alikuwa ameketi kwenye sanduku la wakurugenzi na wachezaji kadhaa, ambao wote waliondoka dakika 10 kabla ya kutamatika kwa mechi .
"Sisi ni timu na hiyo inamaanisha mtakaa hadi mwisho," Ten Hag aliiambia Viaplay.
