F Wapiga kura zingatieni kanuni za uchaguzi | Muungwana BLOG

Wapiga kura zingatieni kanuni za uchaguzi



Na Timothy Itembe Mara.

Wajumbe na wapiga kura wa Chama cha mapinduzi(CCM)wametakiwa kupiga kura kwa kuzingatia maadili na kanuni za uchaguzi ili kuondokana na tabia ya kupiga kura kwa kufuata maelelezo ya viongozi ambao wanatumia mwanya huo kuwatumia kwa masilahi yao binafsi.

Akiongea mwenyekiti mstaafu ccm kata Nyamisangura,Haruni Nyangwe alisema kuna baadhi ya wajumbe na wapiga kura ndani ya chama wanapiga kura kwa kufuata maelekezo ya viongozi wasiokuwa waaminifu na wasio na maadili ambao wanawataka kupiga kura kwa maelekezo jambo ambalo halileti heshima kwenye Chama.

Mwenyekiti alisema hayo jana pindi alipokuwa akijiuzulu nafasi aliyokuwa nayo ili kupisha kura ziumane ndani ya chama hicho za kuwachagua viongozi mbalimbali akiwemo mwenyekiti mpya.

“Mimi niwaombe ndugu zangu wajumbe ondokeni na tabia ya kuwa nyuma ya wagombea wenye masilahi yao binafsi ambao wanatoa kitu kidogo kwa wapiga kura ili kuwapigia kura watu waliowasimamisha kufanya hivyo ni kupiga kura kwa maelekezo ya mtu na atakutumikisha miaka yote kwa sababu ulipokea kitu kidogo”alisema Nyangwe.

Kiongozi huyo alibainisha kuwa badala ya wajumbe kupiga kura kwa maelekezo ya mtu na kuwa watumwa kuna haja wazingatie kanuni za uchaguzi huku wakufuata taratibu zilizopo za uchaguzi ndani ya chama chake  kwa  mjibu wa sheria.

Kiongozi huyo alimaliza kwa kuwataka vijana na wajumbe wapiga kura kwa ujumla kufanya kazi ya kuwaingizia kipato na kuondokana na kuwategemezi ya kutumiwa na baadhi ya viongozi wenye nia ovu kwa madai kuwa wanapanga safu badala yake wapiga kura wafuate maelekezo ya katiba ya uchaguzi na kanunia zake.

Katika uchaguzi ndani ya kata Nyamisangura msimamizi wa uchaguzi,diwani CCM kata ya Bomani,Gotora Philimoni Gotora aliwataja washindi kuwa ni Daniel Cheo Chagini aliyeshinda nafasi ya mwenyekiti na kupata kura 74 na kuwashinda Ayubu Gitinkwi aliyepata kura 15 huku mgombea Mwihechi Marwa Mwihechi akiambuliakura7.

Wengine waliochaguliwa kwa mjibu wa msimamizi wa uchaguzi ni pamoja na katibu ccm kata Nyamisangura Charles Mariba aliyepata kura 25,katibu mwenezi aliyechaguliwa Mussa Bina mwakilishi mkutano mkuu mkoa Godwini Mhoza.

 

Post a Comment

0 Comments