Vita vya Ukraine:Poland kutuma ndege nne za kivita Ukraine 'katika siku zijazo'


Poland itatuma ndege nne za maoigano za aina ya Mig jetza enzi ya Usovieti nchini Ukraine – na kuwanchi ya kwanza ya Nato kutuma ndege zaketangu Urusi uanze uvamizi wa Urusi nchini Ukraine .


Rais wa Poland Andrzej Duda alisema kwamba ndege hizo zitapelekwa katika siku zijazo, na nyingine zitapelekwa baadaye.


Ingawa msada huo unapokelewa vyema kwa maana kwamba utaboresha utendaji wa kikosi cha ulinzi wa anga cha Ukraine, jeti hizi za ziada hazitarajii kuleta mabadiliko yoyote katika vita.


Naibu spika wa bunge la Ukraine Olena Kondratyuk amesema kuwa anatumaini nchi zaidi zitafuata mfano wa Poland.


Nchi nyingine za Nato zinaangalia uwezekano wa kutuma ndege za enzi ya Usovieti, ambazo ndizo marubani wa Ukraine wamefunzwa kuzitumia .


Awali Ukraine iliyaomba mataifa ya Magharibi kuipatia ndege za kisasa za aina ya jeti kama vile F-16.


Uingereza inawapatia mafunzo marubani wa Ukraine kuhusu uendeshwaji wa ndege zenye viwango vya NATO.Lakini kwasabababu ya mafunzo ya kipindi kirefu, imeonya kuwa kupeleka jeti za Magharibi nchini Ukraine utakuwa ni mpango wa baadaye.

Post a Comment

0 Comments