Waficha maiti kuepuka ghalama za kufuata huduma ya Mochwari

 


Njombe


Wananchi wa kata ya Kifanya halmashauri ya mji wa Njombe wanadaiwa kuficha taarifa za vifo vya wapendwa wao wanapofariki nyakati za jioni au usiku ili kuepuka ghalama za kusafirisha miili zaidi KM 50 mpaka Mochwari iliyopo hospitali ya mji wa Njombe Kibena.


Hayo yamebainishwa kwenye mdahalo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa za mradi wa kuzingatia matumizi ya jamii kwenye sekta ya afya (PETS) unaofadhiliwa na shirika la foundation for Civil Society unaotekelezwa na shirika la Highland Hope Umbrella (HHU) katika kata ya Kifanya.


"Kata nzima ya Kifanya haina mochwari na kama mnavyojua serikali ilipiga marufuku na wapendwa wetu wanaoweka duniani adha hii imesababisha wananchi kujiongeza mtu anapofariki na kusema mgonjwa amezidiwa kumbe ameshaaga dunia ili kuepuka ghalama za kuutoa mwili kutoka Kifanya,kwa hiyo taarifa ya mgonjwa kufariki anaanza kuugua. kesho yake asubuhi"alisema Kelvin Mwinuka mratibu wa mradi.


Shigela Ganja ni mchumi wa halmashauri ya mji wa Njombe, kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri katika mdahalo huo amekiri uwepo wa changamoto ya Mochwari katika kata ya Kifanya huku akibainisha kuwa halmashauri inajenga vituo vingi vya afya kwa ndani hivyo wanaamini changamoto hizo.


"Ni kweli ukienda pale wananchi wanataka mochwari yaani hata bila hayo majengo ya nyumba na nini mkiuliza mnataka nini wanakwambia Mochwari lakini niwahakikishie tuna miradi,vituo karibu vitano vinatumia matumizi ya ndani vyote hivyo tunaingiza fedha"alisema Ganja.


Aidha katika maadhimio ya mdahalo baadhi ya baadhi ya wajumbe wakiwemo wenyeviti vijiji kutoka kwa hiyo licha ya wengine wameomba kujengwa Mochwari katika kituo cha afya Kifanya ili kuondoa adha wanayokutana nayo wananchi.

Post a Comment

0 Comments