https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mzozo wa Sudan: Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 85 atelekezwa kando ya ubalozi wa Uingereza | Muungwana BLOG
https://monetag.com/?ref_id=TTIb

Mzozo wa Sudan: Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 85 atelekezwa kando ya ubalozi wa Uingereza


 Raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 85 nchini Sudan alipigwa risasi na walenga shabaha na mkewe akafa kwa njaa baada ya kuachwa wajitegemea na ubalozi wa Uingereza nchini Sudan, familia yao imeambia BBC News Arabic.


Abdalla Sholgami aliishi na mke wake mwenye umri wa miaka 80, Alaweya Rishwan, kando ya mkabala na balozi wa Uingereza mjini Khartoum.


Lakini licha ya wito wa mara kwa mara wa kuomba msaada, mmiliki wa hoteli ya London hakuwahi kupewa usaidizi wa kuondoka Sudan, hata wakati timu ya kijeshi ya Uingereza ilipotumwa kuwahamisha wafanyakazi wa kidiplomasia.


Badala yake, wanandoa hao wazee waliambiwa waende kwenye uwanja wa ndege ulioko kilomita 40 nje ya Khartoum - ambayo ingemaanisha kuvuka eneo la vita - ili kupanda ndege ya kuwahamisha.


Ofisi ya mambo ya nje ya Uingereza ilikiri kwa BBC kwamba hali ya Sholgamis ilikuwa "ya kusikitisha sana" lakini ikaongeza kuwa "uwezo wetu wa kutoa usaidizi wa kibalozi ni mdogo sana na hatuwezi kutoa usaidizi wa kibinafsi ndani ya Sudan".


Eneo kidiplomasia la Khartoum limeshuhudia mapigano makali tangu mzozo huo ulipozuka tarehe 15 Aprili.

Post a Comment

0 Comments