Papa Francis aondoka katika hadhira ya Ijumaa kwa homa

 


Papa Francis amejiondoa katika hadhira yake ya Ijumaa baada ya kuugua homa, msemaji wa Vatican amesema.


Matteo Bruni aliwaambia waandishi wa habari kuwa kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki anajisikia vibaya. Hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi.


Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 86 amekumbwa na matatizo mengi ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni.


Mnamo Aprili, alikaa siku kadhaa hospitalini baada ya kuugua maambukizi ya njia ya kupumua


"Kutokana na homa, Papa Francis hakujitokeza mbele ya hadhira asubuhi ya leo," Bw Bruni alisema akijibu swali la mwandishi wa habari. Haikuwa wazi kama Papa atahudhuria hadhira ya faragha siku ya Jumamosi.

Post a Comment

0 Comments