Mfumo wa malipo ya vibali vya usafirishaji mbao wakwamisha malori Njombe


Zaidi ya malori mia mbili yaliyobeba mbao mkoani Njombe, yamekwama kuondoka kwa zaidi ya wiki moja, kwa kile kinachodaiwa ‘kukwama kwa mfumo’ wa malipo ya tozo za vibali katika usafirishaji wa mazao hayo ya misitu.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka,baadhi ya wafanyabiashara wa mbao, wamesema hi ini mara ya pili kwa tatizo hilo kujitokeza ambapo mara ya kwanza ilikua mwezi July mwaka huu.

Kwa mujibu wa malalamiko yao, licha kulipia tozo hizo kwa mtandao, pale wanapofuatilia vibari ndipo shida huanza, kwani huambiwa na mamlaka husika kuwa “mfumo unasumbua,” jambo ambalo husababisha washindwe kushafirisha shehena hiyo ya mbao.

Kwa nyakati tofauti, Sophia Raymond na Subira Kyando ambao ni sehemu ya wafanyabiashara hao, wamemuomba RC Mtaka kuwasaidia katika kupunguza vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu, wakidai siyo tu vimekuwa vikileta usumbufu, lakini pia vinachukua ambao ungetumika safarini.

Kwa upande wake, Wakala wa Misitu mkoani humo, Audatus Kashamakula, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kudai kuwa imetokana na kusimama kwa mifumo wa utozaji kodi wa Wizara ya Fedha, jambo ambalo lipo nje ya uwezo wao.

"Nawaomba radhi wadau wetu wa mazao ya misitu, hili ambalo limetokea. Tulifanyia kazi pamoja na changamoto zote ambazo zimetokea hasa mfumo ambao ulikuwa haujakaa sawa," amesema Kashamakula.

RC Mtaka amezitaka mamlaka husika kushughulikia suala hilo kwa haraka huku akisema: “Uchumi wa Njombe kwa zaidi ya asilimia sabini, unategemea mazao yatokanayo na misitu, hivyo inatulazimu kuwa na usimamizi mzuri, tunao wajibu kunaweka mazingira mazuri ya biashara kuliko kuwaza kukusanya tu,” amesema.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items