Husna Hassan,Mtwara.
Serikali imesema kuwa vijiji vyote vilivyopo Mkoa wa Mtwara 758 mpaka kufika mwezi disemba 2023 vijiji hivyo vitafikiwa na huduma ya umeme.
Hayo yameelezwa leo Septemba 21,2023 na Naibu Waziri wa Nishati Judithi Kapinga alipofanya ziara fupi ofisini kwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara ziara hio ikiwa na lengo na kutembelea,kuona wakandarasi wanavyofanya kazi lakini pia kuwasha umeme katika vijiji ambavyo huduma hio imefika pamoja na kusikiliza changamoto za wana nchi wakati wa kuunganisha umeme katika miradi ambayo inatekelezwa na serikali
“Hali ya uzalishaji wa umeme kwa Mkoa wa Mtwara kidogo imesua na ni kwasababu kuna matengenezo ambayo yanaendelea na na tunategemea baada ya matengenezo kukamilika basi hali ya uzalishaji ya umeme itaendelea kuimarika “
“ lakini vilevile ninatarajia kwenda kutembelea miradi yetu ya rea yakupeleka umeme vijijini awamu ya 3 mzunguko wa 2 ambapo katika vijiji vyote vya Mtwara 758 vijiji vingi vilikua havina umeme na tumepeleka umeme katika maeneo hayo na mpaka kufika mwezi disemba vijiji vyote vitapata umeme “amesema Naibu Waziri wa Nishati
Aidha Mh Judith ameongeza kuwa azma ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana kwa wa Tanzania wote ili kuchagiza shughuli za maendeleo.
