Halina mada

 


Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman anasema hajali shutuma za 'kijitakasa kimichezo'.


Taifa hilo la Ghuba limeshutumiwa kwa kuwekeza katika michezo na kutumia matukio ya hali ya juu ili kuboresha sifa yake ya kimataifa.


Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudi Arabia (PIF) uliongoza kuinunua klabu ya Newcastle United mwaka jana na kuzindua LIV Golf.


"Ikiwa kujitakasa kimishezo kutaongeza Pato la Taifa langu kwa 1%, basi tutaendelea kufanya hivo," Bin Salman alisema.


Aliiambia Fox News: "Sijali [kuhusu muda]. Nina ukuaji wa 1% katika Pato la Taifa kutokana na michezo na ninalenga 1.5% nyingine.


Saudi Arabia imekosolewa kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu - wanaume 81 walinyongwa siku moja mwaka jana - ukiukwaji wa haki za wanawake, kuharamisha ushoga, kizuizi cha uhuru wa kujieleza na vita nchini Yemen.


Msimamo wake wa kimataifa uliharibiwa vibaya na mauaji ya 2018 ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa Saudi anayeishi Marekani ambaye alikuwa mkosoaji maarufu wa serikali.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items