Hamas waishtumu Israel kwa kukiuka makubaliano ya muda ya kusitisha vita

 


Mshauri wa vyombo vya habari kwa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Taher Al-Nono, anasema kwamba kulikuwa na "ukiukaji" ndani ya makubaliano ya usuluhishi wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, ambayo yalianza kutekelezwa Ijumaa asubuhi.


Al-Nono alisema kuwa wanajeshi wa Israel "walikiuka makubaliano ya kusitisha mapigano," huku wakifyatua risasi dhidi Wapalestina wakati wa kipindi cha kusitisha mapigano, kusababisha kuuawa kwa Wapalestina wawili mjini Gaza.


Alisema kuwa msaada ulioingia katika eneo la kaskazini mwa Gaza ni "mdogo sana kuliko ilivyokubaliwa."


Aliongeza kuwa Hamas "inafuatilia utekelezaji wa kila kifungu cha makubaliano kwa undani," lakini Israel "inatishia" utekelezaji wa makubaliano hayo kikamilifu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items