Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) katika kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana, Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania, imeidhinisha Waraka wa Matarajio wa TCCIA Investment Plc kuuza hisa za upendeleo 72,957,660 kwa wanahisa wake kwa bei ya Shilingi 145 kwa kila hisa.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo Novemba 16, 2023 wakati wa uzinduzi wa Hisa za Upendeleo, Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Bw. Nicodemus Mkama amesema TCCIA Investiment Plc imekidhi vigezo vya kuuza hisa hizo hivyo kampuni na taasisi katika sekta za umma watumie fursa katika masoko ya mitaji kupata fedha za kugharamia shughuli za kibiashara na miradi ya maendeleo.
"Kuhudhuria kwenu ni uthibitisho kwamba kampuni ya TCCIA ina wadau wengi wanaounga mkono juhudi za kukuza mtaji na shughuli za kampuni, na hivyo kuchochea ukuaji wa sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji, na uchumi kwa ujumla hapa nchini'' amesema CPA Mkama
''Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ina jukumu la kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kiutendaji ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharamia shughuli za maendeleo''
Pia, uwepo wa bidhaa nyingi katika masoko ya mitaji unachangia utekelezaji wa Sera za Fedha katika Uchumi na Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, kuongezeka kwa akiba hapa nchini, kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira, Mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla.
CPA Mkama amesema kazi hiyo haikuwa ndogo na rahisi lakini wameweza kufanya kazi yao vizuri na kufanikisha hatua hii kwa weledi na kwa ufanisi mkubwa, na hivyo kupata idhini kutoka CMSA.
Aidha CMSA itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma, hatifungani za miundombinu.
Hatifungani rafiki wa mazingira, hatifungani za bluu, hatifungani za jamii na hatifungani za taasisi za Serikali huku akitoa rai kwa kampuni na taasisi katika sekta binafsi na umma kutumia fursa katika masoko ya mitaji kupata fedha za kugharamia shughuli za kibiashara na miradi ya maendeleo.
''Hatua hii ni muhimu kwa ustawi wa kampuni, ukuaji wa sekta fedha na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu, hivyo naomba mauzo haya yafanyike kwa mafanikio'' amesema Bw. MkamaMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCCIA Investment Plc; Dkt. Fortunatus Magambo akizumza wakati wa uzinduzi wa hisa za upendeleo leo Novemba 16, 2023 jiji Dar es salaam.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TCCIA Investiment Plc Bw. Fortunatus Magambo amesema ili kufikia malengo kampuni hiyo imedhamiria kupanua wigo wa uwekezaji kwa kuwekeza hisa kwenye makampuni ambayo yamejiorodhesha kwenye soko la hisa la Dar es salaam, Afrika Mashariki pamoja na nchini za kusini mwa Afrika.
''Tunawakaribisha wanahisa wetu kushiriki kwenye zoezi hili la ununuzi wa hisa za upendeleo ili kufikia malengo yetu kupata shilingi bilioni 10.58 ili tuweze kuingia kwenye masoko mengine taja hapo juu'' ameongeza Bw. Magambo
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE
Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama akizungumza jambo katika hafla hiyo.


.jpeg)

.jpeg)

