Na John Walter-Manyara
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mjini Babati imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kuboresha Sekta ya afya ili wananchi wapate huduma bora.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) mjini Babati Eva Luoga baada ya kufanya ziara katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Babati kutembelea wagonjwa katika wodi ya wanawake na kutoa misaada mbalimbali.
UWT Babati mjini wamejionea wodi mpya ya kisasa ya kinamama na watoto iliyosaidia kuondoa changamoto ya wanawake kushirikiana kitanda wanapofika kupata huduma.
Jumuiya hiyo imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwa Mwenyekiti wao wa taifa Marry chatanda na Makamu wake Zainabu shomari.
Luoga ameeleza kuwa wametembea wodi ya wazazi kuwafariji wanawake wenzao waliojifungua, wajawazito na watoto njiti na kuridhishwa na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.
