Hamas imedai kuwa watu wenye silaha waliotekeleza shambulio la risasi mjini Jerusalem asubuhi ya leo na kuwaua watu watatu ni wanachama wake, kwa mujibu wa kituo cha Telegram chenye uhusiano na kundi hilo.
Katika taarifa, Hamas ilisema kwamba "operesheni hiyo ilikuja kama jibu la kawaida kwa uhalifu ambao haujawahi kutokea," ikitoa mfano wa kampeni ya kijeshi ya Israeli huko Gaza na mateso ya wafungwa wa Kipalestina katika jela za Israeli.
Taarifa hiyo pia ilitoa wito wa "kuongezeka kwa upinzani," shirika la habari la AFP lilisema.
