Mwanajeshi akamatwa akijaribu kumwachilia waziri anayeshikiliwa Guinea-Bissau

 


Mwanaume mmoja anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi la wanajeshi waliojaribu kumwachilia waziri anayeshikiliwa na afisa mkuu wa serikali nchini Guinea-Bissau amekamatwa, jeshi linasema.


Milio ya risasi kali iliripotiwa katika mji mkuu Bissau siku ya Ijumaa asubuhi.


Walinzi wa Kitaifa walikuwa wamewachukua maafisa hao kabla ya kutafuta kimbilio katika kambi kusini mwa jiji.


Vikosi maalumu viliingilia kati baada ya majaribio ya mazungumzo kushindikana, na kusababisha kurushiana risasi. Utulivu unasemekana kurejeshwa baadaye.


Siku ya Jumamosi, Rais Umaro Sissoco Embalo alisema ghasia hizo ni "jaribio la mapinduzi", akitahadharisha "madhara makubwa" kwa wahusika.


Alikuwa akizungumza baada ya kurejea kutoka katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa wa COP28 huko Dubai.


Waziri wa Fedha Souleiman Seidi na António Monteiro, katibu wa serikali wa hazina, walikuwa wamezuiliwa huku kukiwa na uchunguzi wa madai ya uondoaji usio wa kawaida wa $10m (£8m) ya fedha za serikali.


Walihojiwa Alhamisi alasiri na uchunguzi dhidi ya ufisadi ili kufafanua malipo kwa kampuni 11.


Katika kikao cha bunge siku ya Jumatatu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo alidai kuwa wamiliki wa kampuni hizo walikuwa karibu na viongozi wa muungano unaotawala nchini humo.


Bw.Seidi alitetea malipo hayo kuwa halali. Siku ya Alhamisi baada ya kuhojiwa, Bw Seidi na Bw Monteiro walikamatwa na kuzuiliwa ili wasije kuharibu uchunguzi, vyombo vya habari vya ndani vilisema.


Wanajeshi wa Walinzi wa Kitaifa baadaye jioni walivamia seli za polisi, zilizo karibu na soko la Bandim, "wakiwa na silaha za AK-47 na bazoka" na kuwaondoa maafisa waliozuiliwa, chombo cha habari cha binafsi cha O Democrata kiliripoti.


Ilisema Walinzi wa Kitaifa waliwapeleka mahali pasipojulikana. Siku ya Ijumaa asubuhi, vikosi vya kuleta utulivu vya kikanda vilivyotumwa na jumuiya ya kikanda ya Afrika Magharibi Ecowas vilionekana vikishika doria mitaani, shirika la habari la AFP liliripoti.


Guinea-Bissau imekumbwa na mfululizo wa mapinduzi na majaribio ya mapinduzi tangu kupata uhuru kutoka kwa Ureno mwaka 1974.


Mwezi Februari mwaka jana, rais alisema alinusurika katika jaribio la mapinduzi baada ya kupigwa risasi nyingi kwa saa tano katika tukio ambalo watu 11 walikufa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items

Kilimo cha Bamia