Rufaa dhidi ya Paulina Gekul yatupwa mbali.Na John Walter- Manyara

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara mbele ya Mheshimiwa Jaji Devotha Kamuzora imetupilia mbali Shauri la rufaa ya jinai namba 577 la mwaka 2024 iliyokuwa inamuhusu Hashimu Ally ambaye ni mrufani dhidi ya Paulina Gekul ambaye alikuwa ni mrufaniwa.

Kwa upande wake wakili wa Hashimu Ally, Peter Madeleka amesema hajaridhishwa na maamuzi hayo kwani kuna madudu yanaendelea kwenye kesi hiyo, hivyo ndani ya siku mbili watahakikisha wanakata rufaa, ili haki dhidi ya mteja wake itendeke.

Naye wakili wa Pauline Gekul, Efraim Kisanga amesema maamuzi yaliyotolewa na Jaji Devotha ni sahihi, hivyo muda wowote kuanzia sasa mteja wake atafungua kesi ya madai kwa wale wote waliomchafua kupitia kashfa hiyo na ukweli wote utajulikana ndani ya muda mfupi.

Katika rufaa hiyo Hashimu Ally anapinga uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Desemba 27, 2023 ya kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Post a Comment

0 Comments