Dkt. Yonazi aongoza kikao cha Makatibu Wakuu cha Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



Na.Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi  ameongoza kikao cha Makatibu Wakuu kuhusu Tathmini ya Maadhimisho ya Sherehe ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa Jijini Dar es Salaam Aprili 26, 2024 pamoja na Maandalizi ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa itakayifanyika 25 Julai 2024.


Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika  katika ukumbi wa Ofisi yake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki na kuhusisha baadhi ya makatibu wakuu Dkt. Yonazi amepongeza na kuwashukuru timu zima ya kamati tendaji kwa namna ilivyotekeleza jukumu hilo na kufanikisha sherehe mbalimbali za Kitaifa nchini.

Dkt. Yonazi amesema kuwa Ofisi yake itaendelea kuratibu sherehe hizo kwa mujibu wa taratibu zilizopo na kuhakikisha sherehe zinafanikiwa kwa ufanisi na ubunifu zaidi ili kuendelea kuenzi na kuwa na kumbukumbu za Matukio hayo makubwa kwa Kitaifa.

Aidha ametumia kikao hicho kukikumbusha Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kuendelea kufanya kazi kwa uzalendo na kuzingatia taratibu za utendaji kazi wa Serikalini.


Post a Comment

0 Comments