Sillo akabidhi magari mawili tarafa ya Mbugwe.



Na John Walter-Babati

Wananchi zaidi ya laki mbili wa tarafa ya Mbugwe wilaya ya Babati mkoani Manyara wanakwenda kunufaika na magari ya wagonjwa wa dharura yaliyotolewa na Serikali.

Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Babati Dr Hosea Madama amesema kabla ya gari hilo,walikuwa wakitumia gari dogo Suzuki marot moja ambalo lipo kituo cha Afya Magugu, hivyo wanamshukuru Rai Samia Suluhu Hassan na Mbunge kwa kuhakikisha magari hayo yanapatikana.

Amesema kwa sasa wamepata magari mawili ya wagonjwa, moja limeshakabidhiwa  tarafa ya Bashnet na kwa sasa huitaji zaidi ni tarafa ya Ghorowa na Babati. 

Magari hayo mawili yamekabidhiwa leo Mei 18,2024 na Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo-naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa chama, serikali na wananchi.

Kati ya magari hayo, moja ni kwa ajili ya wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya wilaya iliyopo kata ya Mwada tarafa ya Mbugwe na lingine kwa ajili usimamizi huduma za afya kwenye vituo ambapo thamani yake ni shilingi milioni 400.



Sillo ameitaka Halmashauri ikayasimamie magari hayo ili yatoe huduma inayotarajiwa kwa wananchi.

“Mheshimiwa Rais Samia anawapenda ndo maana ametoa magari haya yakatoe huduma ya kubebea wagonjwa na kuwaleta kwenye huduma kwa haraka" alisema Sillo 

Sillo amesema serikali imeendelea kuboresha sekta ya afya ambapo imejenga Hospitali ya wilaya ya Babati kwa zaidi ya shilingi bilioni 3.326, vituo vya afya kata ya Madunga, Bashnet, Ayasanda na Gidas kwa shilingi Bilioni 1.75 na kwa sasa zinasubiriwa milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Kata ya Kiru na kwamba shilingi milioni 450 zimetolewa kwenye zahanati tisa.

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Babati Mheshimiwa Jackson Hhaibey, amesema magari hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa wananchi hivyo yatumike kama ilivyokusudiwa.

Amesema ni heshima kubwa kuwa na Mbunge anayekubalika na watu na kuaminika na serikali na ndia maana kapewa nafasi ya kuwa Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi.

Post a Comment

0 Comments