UVCCM Babati vijijini watakiwa kugombea nafasi mbalimbali.



Na  John Walter -Babati

Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UVCCM) Wilaya ya Babati vijijini, wametakiwa kujiamini na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu 2025.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya  Babati Mheshimiwa Jackson Hhaibey wakati akizungumza na Vijana katika baraza lao lililoketi leo mei 18,2024.

Aidha amewataka kuendelea kuwa na nidhamu waliojengewa na Viongozi wao katika kambi ya Singe kwani ndo msingi wa uongozi bora.

Baraza hilo likiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Manyara Mheshimiwa Inyasi Amsi, lililenga kutoa mwongozo na dira kwa vijana kuhusiana na kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika chaguzi zilizoko mbeleni lakini pia kuwakumbusha kujiunga kwenye mfumo wa kielektroniki.



Inyasi amesema watajitahidi kutafuta viongozi wenye sifa na uwezo ambao hawatamuangusha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na kile ambacho mama amewaonesha kwa kuwapa vijana kipaumbele kwenye nyanja mbalimbali za uongozi.



Mbunge wa Vijana Asia Halamga amesema ili vijana kufikia malengo yao katika chama cha Mapinduzi ni lazima kushirikiana na kupendana na kwamba ambaye hayupo tayari hawana budi kuachana naye.



Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo amempongeza mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Manyara kwa kufanya mabaraza ya Vijana katika wilaya zote za mkoa huo kwa kuwa inaongeza ari kwao kukipenda Chama cha Mapinduzi.

Sillo amewataka vijana wasikubali kuona au kusikia viongozi wa baadhi ya vyama vya upinzani wanaosimama majukwaani na mitandaoni kuwatukana Viongozi akiwemo Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.


Post a Comment

0 Comments