Airtel Tanzania yatoa gawio la zaidi ya TZS bilioni 40 kwa Serikali


Dar es Salaam, Juni 11, 2024. Airtel Tanzania leo imekabidhi hundi ya TZS 40,842,742,033.15 kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni malipo ya gawio la mwaka wa fedha 2023/24. Gawio la Airtel kwa serikali limewasilishwa leo katika hafla maalum ya Siku ya Gawio la Mwaka 2024 iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina Ikulu jijini Dar es salaam. Hafla ya hiyo makabidhiano ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kupitia hafla ya Kugawa Gawio kwa serikali  Airtel Tanzania ni miongoni mwa kampuni za biashara tatu zilitoa kiasi kikubwa cha Gawio mwaka huu kati ya kampuni za biashara ambazo serikali ina hisa ndani yake kwa mwaka huu. Tangu mwaka 2019, Airtel Tanzania Plc na Airtel Money Tanzania Limited zimekuwa zikitoa Gawio kwa Serikali ikiwa ni matokeo ya jitihada za Airtel katika kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa. Serikali inaumiliki wa hisa asilimia 49 ndani ya Airtel Tanzania, ambapo kutokana na utaratibu huu wake wa  kutoa Gawio kwa serikali tayari Airtel imelipa gawio la zaidi ya TZS 200 bilioni, na hivyo kudhihirisha nafasi ya ubia wake kama    mshirika  anayechochea maendeleo nchini  wa Tanzania.

Akizungumzia  hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na wadau wa sekta mbalimbali za maendeleo, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Eliud Sanga alieleza kuwa Airtel Tanzania inawekeza katika ukuaji wa taifa kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika teknolojia na mawasiliano.

“Mikakati madhubuti ya   serikali katika  kushughulikia changamoto za uwekezaji na sera Madhubuti zimejenga  mazingira bora hata kwentu Airtel katika  kustawisha bishara na kukabiliana na soko la ushindani, kwa hilo tunatoa shukrani zetu” alisema.

Sanga aliongeza kuwa, Airtel inafanya kazi bega kwa bega na serikali katika kusambaza bidhaa na huduma kwa gharama  nafuu na kulingana na mahitaji ya wateja . Pia alizungumzia mradi waliozindua hivi karibuni wa Airtel Tanzania katika kuendeleza ajenda ya serikali ya elimu ya kidijitali. “Mfano mzuri ni mradi wa Airtel kinara wa ‘Airtel SMARTWASOMI’ uliozinduliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa msaada wa UNICEF na Wizara ya Elimu na Wizara ya Serikali za Mitaa”.

“Airtel SMARTWASOMI imezinganisha na mtandao wa Intaneti  shule 50 za sekondari zilizopo Zanzibar, Dodoma, na Mbeya kuwa madarasa mahiri, na kunufaisha zaidi ya wanafunzi 55,000 na kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 2,000. Miradi kama hii inadhhirisha  dhamira yetu ya kutumia teknolojia kwa maendeleo bora ya elimu na kukamilisha mpango wa serikali  katika kutoa elimu bila malipo kwa kila mtoto”, alisema Sanga.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Dinesh Balsingh alieleza kuwa gawio iliyowasilishwa mbele ya Mh. Dk. Samia Suluhu Hassan inadhihirisha dhamira  ya kampuni Airtel  katika ustawi wa uchumi wa Tanzania. Balsingh  alisisitiza umuhimu wa kuongeza matumizi na uwepo wa  simu za janja  ili kuongeza kasi vijana kutumia huduma za data na huduma za kifedha kwa maendeleo yan chi.

“Ahadi yetu kama Airtel Tanzania ni kutoa huduma za mawasiliano kwa urahisi na kwa gharama  nafuu. Tunazidi kujionea jinsi gani ongezeko la matumizi ya simu janja zinavyochangia na kuchochoea upatikanaji wa taarifa kwa vijana na huduma za kifedha,” alieleza Balsingh.

Balsingh aliongeza zaidi “Idadi ya watumiaji wa simu nchini Tanzania imeongezeka kwa kiasi kikubwa, Hii ni kufatia ripoti ya GSMA, ambapo asilimia 72 ya Watanzania wanatumia huduma za fedha kwa njia ya simu, na hivyo teknolojia inaendelea kutoa masuluhisho  mbalimbali ikiwemo hii ya  kupanua upatikanaji wa fedha nchini.”

Notes to Editor:
About Airtel
Airtel Africa is a leading provider of telecommunications and mobile money services, with a presence in 14 countries in Africa, primarily in East Africa and Central and West Africa. Airtel Africa offers an integrated suite of telecom solutions to its subscribers, including mobile voice and data services as well as mobile money services, both nationally and internationally. We aim to continue providing a simple and intuitive customer experience through streamlined customer journeys.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items