NSSF waja na huduma mpya NSSF Taarifa

 


REBECA DUWE, TANGA

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii nchini (NSSF) wameshiriki maonyesho ya 11 ya  Biashara na Utalii yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga huku wakiitangaza huduma yao mpya ya NSSF Taarifa.

Akizungumza leo Afisa Matekelezo Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakari Soud Mshangama ambapo alisema mpango huo ni muhimu kwa sababu unamuwezesha mwanachama kupata taarifa binafsi ,michango na madai yake.

Alisema huduma hiyo inapatikana kupitia simu ya kiganjani kwa njia tatu ambazo ni ujumbe mfupi (SMS),Programu ya simu ya Kiganjani (Mobile App) ya NSSF na WhatApp.

“Leo tupo hapa kwenye maonyesho haya pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma zetu lakini pia tunatumia kuitangaza Programu hii ambayo  inamuwezesha mwanachama kupata taarifa na huduma mbalimbali kwa njia ya ujumbe mfupi”Alisema.

Aidha alisema pia walikuwa wakieleza mafao yanayotolewa na Mfuko huo na vigezo vyake ikiwemo Mafao ya Pensheni ya Uzeeni ambayo mwanachama hulipwa kila mwezi kwa anayetimiza vigezo vilivyowekwa.

Awali akizungumza mara baada ya kutembelea Banda la NSSF Mkuu wa wilaya ya Muheza Zainab Abdallah alisema kuwa  NSSF ni muhimu sana huku akiendelea kuwataka wafanyakazi na wasiowafanyakazi kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na mafao mbalimbali ikiwemo ya matibabu,dharura kama wamepata magonjwa hivyo wanapoweka akiba yako ikitokea umepata jambo lolote ni rahisi kukuhudumia.

Alisema wanapoweka akiba yako inakuwa ni rahisi unapokumbana na changamoto mbalimbali inakuwa ni rahisi kuweza kukuhudumia na kukupa matibabu ikiwemo unapofikia umri wa kustaafu unaweza kuwa na akiba yako ambayo inaweza kukulea mwenyewe.

“Niendelee kuwahimiza wafanyakazi na waajiri wajue kwamba ni takwa la kisheria wahakikisha wanawaingiza watumishi kwenye mfuko wa hifadhi za Jamii (NSSF) ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali ”Alisema

Post a Comment

0 Comments