TRA yawataka wananchi kutoa ushirkiano kupata elimu ya mlipa kodi

 


Na Rebeca Duwe Tanga.


Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imetoa wito  kwa wananchi wa Mkoa Tanga kutoa ushirikiano ili kuweza kupata Elimu kwa walipa kodi ambayo hutolewa bure  na mamlaka hiyo pamoja na huduma ya TN.

Hayo yamebainishwa na Flavian Byabato ambaye Afìsa mkuu msimamizi wa kodi TRA wakati akizungumza waandishi wa habari katika Banda la TRA kwenye Maonyesho ya Biashara na Utalii ya 11 yaliyofanyika katika viwanja vya shule sekondari Usagara Jijini Tanga.

Aidha alisema kuwa lengo la kuwepo wenye maonyesho ni kuweza kuwapa wafanya biashara waliojitokeza kufanya maonesho hayo kuweza kupata huduma zinazotolewa na TRA ikiwemo ushauri na huduma TN na huduma za kidijitali.

Aliongeza kusema kuwa wanafanya huduma ya TN  na makadirio lakini na ushauri juu ya elimu ya digitali kwani maonesho hayo kuna wajasiriamali wiliokuja kuonyesha na kuuza bidhaa zao pengine hawajasajiliwa hivyo watapata huduma hiyo.

Byabato alisema pia wanatoa elimu mifumo lakini elimu ya machine ya EFD  ili wapate utaratibu  upi afuate ili aweze kufuata utaratibu huo.

Post a Comment

0 Comments