Wabunge wananwake kwa kushirikiana na Oryx Gas watoa tuzo kwa Rais Samia


WABUNGE wanawake kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania wametoa tuzo kwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ya kutambua mchango wake katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Tuzo hiyo kwa Rais Dk.Samia imetolewa leo Mjini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Nishati Safi Kupikia Duniani ambako ORYX imeshirikiana na wabunge hao pamoja na wabunge wanaume ambao ni vinara katika nishati safi ambako Spika wa Bunge Dk.Tulia Ackson ametoa sababu za Rais Samia kupewa tuzo ya kumtambua Rais kama kinara wa nishati safi nchini, Afrika na Duniani kwa ujuma.

Dk.Tulia ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema wanampongeza Rais kwa kuwa kinara wa nshati safi ya kupikia. 


Amesema Rais Samia alipokuwa Dubai na hivi karibuni alipoenda katika mkutano uliofanyika Paris ametambulika na dunia nzima kama kinara wa nishati safi ya kupikia.Hivyo wanaendelea kusisitiza Rais Samia ndiye kinara wa nishati safi ya kupikia.

Amesema katika Bara la letu la Afrika kunachangamoto ya nishati ya kupikia na takwimu zinaonesha asilimia 90 barani Afrika wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na ili kutoka katika nishati hiyo na kurudi katika sifrui kabisa itachukua muda.

Hivyo Rais Dk.Samia anasaidia kuupunguza muda kwa kuendelea kutafuta fursa kubadilisha upikaji kwa kuacha kutumia nishati chafu na kuhamia katika nishati safi ya kupikia kama gesi.

Aidha amesema juhudi hizo za Rais zimeanza hapa nchini Tanzania na takwimu nchini zinaonesha asilimia 90 za wananchi mpaka sasa wanatumia nishati isiyo safi ya kupikia na juhudi za Rais zinatusogeza angalau kutoka asilimia 90 na kusogea mpaka 25 ili wawe wachache wanaotumia nishati chafu ya kupikia.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Benoit Araman amesema katika kutambua mchango wa Rais Samia katika nishati safi wameamua kutoa tuzo kwa Rais kama sehemu ya kumuunga mkono kwa juhudi anazofanya huku akisisitiza mpaka sasa wameshatoa mitungi ya gesi na majiko yake 35000 kwa makundi mbalimbali nchini na wataendelea na mkakati wao kwani dhamira yao ni kuona asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2032 kama ambavyo Rais Samia ameelekeza.

Awali Mwenyekiti wa Wabunge Wanawake nchini Shally Raymond amesema wabunge wanawake pamoja na wabunge vinara wa nishati kwa kushirikiana na Oryx wameamua kutoa tuzo kwa Rais huku akitumia nafasi hiyo kupongeza jitihada zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia katika kuhamasisha nishati safi ya kupikia nchini.

Post a Comment

0 Comments