F Mwenge wa uhuru wateketeza dawa za kulevya Kiteto. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwenge wa uhuru wateketeza dawa za kulevya Kiteto.

Na John Walter -Kiteto
Mwenge wa Uhuru ambao unaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, umeteketeza kilo 55 za bangi na mirungi ziilizokamatwa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo. 

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Remidius Mwema, kata ya Njoro inaongoza kwa matukio mengi ya matumizi ya dawa za kulevya wilayani humo.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kiteto na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya. 



Ametoa wito kwa jamii kushiriki katika kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama za watu wanaojihusisha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya ili kuokoa jamii.

Kaulimbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka huu, Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

Post a Comment

0 Comments