Na John Walter -Hanang'
Mradi huo ambao unatekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) umesanifiwa kuhudumia wananchi wapatao 25,000 kwenye vijiji zaidi vinne.
Awali akiweka jiwe la msingi mradi huo kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mnzava alisema kuwa ameridhishwa na mradi huo baada ya kukagua miundombinu, Nyaraka na kuangalia usimamizi ulikuwaje hivyo Mwenge wa Uhuru umejiridhisha na usimamizi wote uliofanyika kwenye mradi huo pasipo na shaka yoyote.
"Nitoe angalizo kwa wananchi ambao tunapata huduma hii muhimu ya maji, tuwe makini kutunza miundombinu hii, tuwe makini kutunza vyanzo vya maji na mabomba ambayo yanatupatia huduma hii muhimu" alisema Mzava
Akisoma taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Meneja wa RUWASA wilaya ya Hanang' Hurbert Kijazi alisema kuwa lengo la mradi huo wa maji ni kuondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kwa wananchi wa Vijiji vya Mogitu, Gehandu, Ming'enyi, Balangdalalu na vijiji jirani.
