Na John Walter -Hanang'
Wanafunzi watatu wa shule ya msingi Nangwa wilaya ya Hanang' mkoani Manyara wamepoteza maisha wakati wakiogelea kwenye bwawa huko kijiji cha Basotushang kata ya Hidet.
Tukio hilo limetokea Oktoba 25,2024 kijijini hapo baada ya Wanafunzi hao kushindwa kuogelea na kuzama bila kupata msaada wowote.
Wanafunzi hao waliofariki ni Alex Joseph January (10), Brayton David Nicomedi (10) na Damiano Paulo Qoda (10).
Wanafunzi hao ni miongoni mwa waliofanya mitihani yao ya darasa la nne Oktoba 24 mwaka huu.
Watoto hao wote umri wapo sawa katika umri wanapishana miezi miwili na mmoja kwa kuwa Alex Joseph January alizaliwa April 13,2014, Brayton David Nicomedi alizaliwa Julai 9,2014 na Damiano Paulo Qoda Mei 1,2014.
Mamia ya Wananchi wamejitikeza Leo katika uwanja wa shule ya msingi Nangwa kuiaga miili ya watoto hao itakayopumzishwa leo.
0 Comments