Mbunge wa Jimbo la Lupembe mkoani Njombe Wakili Edwirn Swalle amehoji wananchi wa jimbo hilo kama kwa sasa anafaa kustaafu kuitumikia nafasi ya uwakilishi Bungeni jambo ambalo limepingwa wakimtaka achukue fomu kwa awamu nyingine.
Swalle ameuliza swali kwa wananchi hao mara baada ya kutoa mrejesho wa kazi zilizofanywa ikiwemo ujenzi wa miradi mbalimbali katika jimbo hilo kwa kipindi chake cha miaka mitano ya uwakilishi ambapo miongoni mwa wananchi aliowahoji ni pamoja na wakazi wa kijiji cha Wanginyi.
"Mkiniangalia Mbunge wenu nafaa kustaafu Ubunge kweli, (hapana) wakijibu wananchi, Ninyi ni watu makini sana na niwaambie wana Wanginyi hizi kero ambazo hatujakamilisha sio kwasababu hatujasema serikalini lakini haya ambayo yamefanywa kwa muda mfupi mnapata picha kwamba tukifanya kwa muda mrefu Wanginyi itakuw bora zaidi"amesema Swalle
Amesema changamoto kubwa ni ujenzi wa barabara ya Kibena kwenda Madeke kwa kiwango cha lami jambo ambalo limesikilizwa na serikali ambapo kwa mara ya kwanza imetangazwa tenda ya ujenzi wa KM 42 katika barabara hiyo.
0 Comments