Kamonga avunja makundi,achukua fomu ya Ubunge Ludewa "Mmenipa changamoto,nitachapa kazi"






Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Joseph Kamonga amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge kwenye jimbo hilo mara baada ya kuteuliwa na chama chake.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 25,2025 Kamonga ameahidi kumaliza changamoto za miundombinu ya barabara katika maeneo ya mwambao wa ziwa Nyasa.

Kamonga amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Ludewa kwa mara nyingine atahakikisha  kero zingine za wananchi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi zinatatuliwa kwa wakati.

"Endapo nitachaguliwa tena kwa miaka mitano mingine kuwawakilisha katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nitahakikisha natatua kero za wananchi wa Ludewa ambazo hazikumalizika" amesema Kamonga.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Ludewa Oscar Simtengu amesema hadi sasa ni mgombea wa chama kimoja tu ambaye amejitokeza kuchukua fomu yavkuwaniavnafasi ya ubunge jimbo la Ludewa.

"Hadi sasa ni mgombea wa chama kimoja tu ndiye amejitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubungevjimbo la Ludewa" amesema Simtengu.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items