F ADC wamuunga mkono mgombea Ubunge Jimbo la Tanga | Muungwana BLOG

ADC wamuunga mkono mgombea Ubunge Jimbo la Tanga

 


NA REBECA DUWE TANGA 

CHAMA cha Alliance for Democratic Change ADC kimesema kinaiunga mkono chama cha wananchi CUF  Kwa kumsimamisha mbunge wa cha hicho Mussa Mbarock ambaye aliyewahi kuwa mbunge wa kwanza wa upinzani katika jiji la Tanga tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama Virginia nchini.

Aidha ilisema wao kama wapinzani wako tayari kuungana wapinzani wengine kuhakikisha wanashika dola ili kuweza kuwapunzisha Chama cha Tawala ambayo imedumu madarakani kwa miaka 64 ya uhuru wa Tanganyika.

Hayo aliyasema mgombea urais Chama cha ADC ,  Mh.Wilson Elias Mulumbe wakati akiwa mkutano wa Kampeni ya chama hicho iliofanyika  katika viwanja vya mabanda ya papa jijini Tanga ,ambapo alisema kuwa wao kama wapinzani ni kuwaunga mkono wapinzani wenzao ili waweze kushika dola kuweza kuwasaidia wananchi katika kero zinazowakabili.

Aidha alimwomba endapo Musa mbarouk atashinda awe mshauri wa serikali kuweza kuchimba mafuta katika bonde la Ufa kabla kuanza kutumia mafuta kutoka nchini Uganda kwa maslahi ya uchumiwa nchi kwani nchi ina rasilimali ya kutosha.

Sambamba na hayo alisema ADC wanakuja na Sera ya matibabu bure katika hospitali zote kwani watanzania  wanahaki ya kupata matibabu bure' lakini pia Elimu kuanzia shule za awali mpaka vyuo vikuu ni bure pamoja na hayo wataondoa mikopo kwa wanachuo ili hata kijana atakapopata ajira asikatwe mshahara wake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa ADC  Taifa alisema kuwa wakipata ridhaa ya kuongoza nchi watauza magari yote ya wanayotembelea viongozi wa serikali  ili wananchi wapate matibabu bure lakini mwananchi akifiwa hatatozwa fedha ya kuchukua maiti badala yake serikali itatoa rambirambi ili mwanchi achukue mwili wa marehemu wake bure .

Naye Musa Mbarouk ambaye ni mgombea ubunge jimbo la Tanga kupitia CUF ambaye ADC inamuunga mkono alisema kuwa atakapopewa ridhaa kuingia Bungeni atapeleka kilio cha kupata madakari Bingwa wa mifupa ikiwa. ni pamoja na matibabu bure kwa wananchi wote  na kuzingatia suala Elimu bure. 

Post a Comment

0 Comments