F CCM Tanga wajiandaa kumpokea mgombea Urais Dkt. Samia | Muungwana BLOG

CCM Tanga wajiandaa kumpokea mgombea Urais Dkt. Samia

 


NA REBECA DUWE ,  TANGA 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye pia mgombea wa urais wa Jamhuri  muungano watanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM  anatarajia  kuingia ndani ya Mkoa wa Tanga tarehe 28 September jion katika eneo la Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akizungumza na waandishi  wa habari katika ofisi za CCM Mkoa waTanga mwenyekiti wa CCM Mkoa  Ostadhi Rajab Abdalrahaman alisema kuwa ujio huo wa mgombea Urais  kupitia CCM unalenga kuzungumza  na Wananchi wa mkoa wa Tanga bila kujali  itikadhi za vyama vyao hivyo ni vyema wananchi kujitokeza ili kuhudhuria kwani kwani ataleta maendelea kwaajili ya wanatanga wote.

Aidha alisema kuwa baada ya Mh.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kupokelewa Mkata atawasalimia wananchi wa mkoa wa Tanga ambapo ataelekea Tanga mjini kwa mapunziko, na tarehe 29 September  ndio atafanya ataanzia ziara yake  katika wilaya ya Pangani kwa muktano wa Hadhara na baadaye atafanya mkutano mkubwa wa hadhara  na wananchi wa Tanga mjini.

Aliongeza kusema kuwa Mh.Rais Dkt Samia  atakuwa ziara ya takribani siku tatu ndani ya mkoa wa Tanga ambapo atapita muheza na Korogwe ambao ratib itaendelea kutolewa ili wananchi wote wapate taarifa juu ya ujuio huo.

"Sisi imani ni kwamba wananchi wataipigia Chama chetu na Daktari Samia suluhu Hassan kwani tumeona maendeleao makubwa kupitia uongozi wa Kiongozi wetu hivyo hakuna kiongozi yeyote ambaye yuko thabiti ambaye  ataleta maendeleo katika mkoa wetu kwaajili ya wananchi wote"alisema Rajabu.

Alisem kuwa kupitia Rais Samia wananchi waendelee kutegemea maendeleo zaidi kwani baada ya ziara yake kikazi aliyoifanya kwa miezi michache iliyopita  amefanya mabadiliko  katika kuhuakikisha miradi ambayo ilikuwa inasuasua sasa inadelea kwa kasi  zaidi.

Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Tanga wametoa maoni yao kuhusu ujio wa Mh.Rais Dkt Samia Suluhu na kusema wananahitaji kwanza kuona aje aone changamoto mbalimbali ikiwemo maisha ya mwananchi mmojommoja na barabara ya pangani pia aikazie mkazo mkubwa zaidi kwani kuna baadhi ya maeneo mvua ikinyesha kunapitika kwa taabu sana.

Boniface Gidion ni moja ya wananchi aliyetoa maoni alisema kuwa ujio wake kama Mgombea urais wa Chama Tawala amesema wao kama wananchi wanatarajia  kuona Dkt.Samia atatatua changamoto ya wananchi mbalimbali lakini pia awangalie na wanyabiashara wadogowadogo wapewe fursa mbalimbali kupitia ujio wake.

Post a Comment

0 Comments