Na Timothy Itembe Tarime.
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tarime mjini kupitia Chama Cha mapinduzi Esther Matiko,amesema wananchi wakimchagua na kuwa Mmbunge atahakikisha mabilioni ya DKT Samia Suluhu Hassani yanawafikia ili kunufaika na kuondokana na mikopo ya kausha damu.
Matiko amesema hayo Leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kata ya Sabasaba ndani ya viwanja vya mazoezi ya mpira wa miguu maarufu Shamba la Bibi ambapo Katibu wa NEC uchumi na fedha wa Chama Cha mapinduzi Taifa,Joshwa Mirumbe.amehudhuria.
Matiko ameongeza kuwa Kuna Kila sababu ya kumpatia kura Mgombea urais kupitia CCM,DKT Samia Suluhu Hassani kwa sababu ndani ya miaka Mine na nusu ametekeleza miradi lukuki Kwa watanzania na pia ana malengo mahususi ya awamu ijayo ikiwemo siku miamoja kutenga fedha shilingi Bilioni 200 ili kupaisha mikopo na wakopaji kuondokana na mikopo ya kausha damu.
Naye Mwenyekiti wa UWT mkoa Mara,Nansi Msafiri alisema kuwa Kwa Mara ya kwanza ndani ya Jimbo letu tuna Mgombea mnyemyekevu na tusimuache amepewa kanzi nzuri na Chama Cha mapinduzi kupeperusha bendera ya CCM siku hiyo tumpe kura pamoja na madiwani wote wanaotokana na Chama Cha mapinduzi.
"tunaye mtuma tunaimami atatufikishia kile tunacho mtuma Kwa Rais wa jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Tangia Uhuru sisi wanawake tumekuwa tukiwaunga wanaume na wanashinda kura awamu hii wanawake na sisi kuamkia Okotoba tuwatii waume zetu tiwabembeleze siku huyo Watuunge mkono kumpa kura DKT Samia Suluhu Hassani Ubunge Esther Matiko na madiwani wanaotolana na CCMalisema Msafiri.
Kwa upande wake Katibu wa NEC uchumi na fedha Chama Cha mapinduzi Taifa,Joshwa Mirumbe alisema anaimami na wagombea wanaotokana na Chama Cha mapinduzi na wananchi wawaamini na kuwapa kura Kwa sababu wakimchagua CCM watakuwa wamechagua maendeleo.
0 Comments