Na Timothy Itembe Tarime.
WAZEE wa Mila wa kabila la wakurya koo 12 wilayani Tarime mkoani Mara wamemtunuku Mgombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini ngao na mkuki kama ishara ya ishujaa.
Abdalha Kaugaga kutoka Kijiji Cha Kenyamosabi alisema kuwa mtu anapo zaa mtoto na kuwa makubwa na kumtahiri akawa mumira anamkabidhi vyombo kama vile silaha ya kujilinda na kulinda Mali ya Watu.
Mzee huyo aliongeza kuwa Katika uzinduzi wa Chama Cha mapinduzi ambao umefanyika Nyamwaga wazee wa Mila wameona ni vyema wamkabishi Mgombea wao Mwita Waitara mkuki na ngao ikiwemo kofia ya jadi kama ishara ya ushujaa Kwa kutekeleza miradi iliyowafurahisha na kuwa vifaa hivyo vikatumike kujilinda na kulinda Mali ya Watu.
Kwa upande wake Mgombea ubunge Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Wilaitara alipongeza hatua ya wazee walioichukia na kutaja sababu iliyomsukuma kutetea nafasi yake ya Ubunge kuwa ni maendeleo aliyoyatekeleza.
Waitara alisema chini ya serikali ya awamu ya sita miradi mingi ya maendeleo imetekelezaka chini ya Raisi wa jamuhuri ya Muungano DKT Samia Suluhu Hassani ikiwemo miradi ya Elimu,Afya,miundombinu ya Barabara na maji Kila Kona.
Katika hatua nyingine Waitara amesema Kwa miaka mitano ijayo kama akifanikiwa kuwa Mbunge ataenda kutetea wananchi wake Bungeni ikiwemo kukamilisha ujenzi wa Chuo Cha VETA kinachojengwa kata ya Matongo Kijiji Cha Nyabichune ili Vijana wakapate ujuzi hapo wa kujiajiri na kuajiriwa Serikalini.
Waitara ameongeza kuwa ndani ya Jimbo la Tarime Vijijini Kuna viongozi 500 kati yake vitongoji 363 vina umeme na tuna vijiji 88 bina umeme nimekuwa nikipiga mahesabu hapa tunapozungumza vitongoji 67 vitongoji 32 tumeisha washa lakini mkandarasi anakusanya vifaa vitongoji 93 tumalize kazi Katika vitongoji 500.
Naye mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi mkoa Mara,Patrick Chandi alisema Wanachama wavunje makundi yaliyokuwepo baada ya uchaguzi wa kura za maoni ili kukipa ushindi Chama hicho Katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Okotoba 29,2025.

