F Mgombea udiwani aiomba Serikali kuutunza mgodi wa Kebaga | Muungwana BLOG

Mgombea udiwani aiomba Serikali kuutunza mgodi wa Kebaga


Na Timothy Itembe Tarime.

MGOMBEA udiwani wa Kata ya Kenyamanyori kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Matiko, amepinga vikali tetesi zinazodai kuwa Mgodi wa Kebaga utachukuliwa na mwekezaji mkubwa kutoka kampuni ya Barrick North Mara Gold Mine. Badala yake, ameiomba serikali kuhakikisha kuwa mgodi huo unabaki kuwa mali ya wachimbaji wadogo wa eneo hilo.

Akizungumza mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Mtaa wa Kebaga Mine leo, Matiko alisisitiza umuhimu wa kuwapa kipaumbele wachimbaji wadogo ambao ndio wamekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa eneo hilo.

Mbali na suala la mgodi, Matiko pia aliwasilisha ombi la uboreshaji wa barabara ya kutoka Kebaga hadi mjini Tarime kwa kiwango cha lami, akieleza kuwa barabara hiyo ni muhimu kiuchumi na italeta maendeleo ya haraka kwa wananchi wa Kenyamanyori na maeneo jirani.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tarime Mjini, Esther Matiko, alisema tayari amekuwa akifuatilia kwa karibu changamoto za wachimbaji wadogo na kuzifikisha bungeni alieleza kuwa lengo si tu kuwapa nafasi ya kuchimba, bali pia kuwasaidia kwa kuwapatia mitaji ya kuwainua kiuchumi.

Katika mkutano huo, Diwani mstaafu wa kipindi cha 2015–2020, Ganga Mgendi, alieleza jinsi alivyokabidhi kata hiyo kwa Diwani Farida Joeli (2020–2025) akiwa ameiacha katika hali ya usalama na utulivu wa kiuongozi ndani ya CCM. Alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Naye Felsta Deogaratuas Njau, ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa CHADEMA kabla ya kujiunga na CCM, aliwataka wananchi kumpa kura Mgombea Urais wa CCM na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa amefanikisha maendeleo makubwa nchini, yakiwemo uboreshaji wa huduma za afya kwa kuongeza vituo vya afya, zahanati, na hospitali, hususan kwa ajili ya mama na mtoto

Post a Comment

0 Comments