Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele amesema nafasi za kujiunga na Mafunzo ya JKT kwa kujitolea Haziuzwi, zinatolewa bure kwa kila kijana wa kitanzania mwenye sifa zilizoainishwa na JKT.
Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo ofisini kwake Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma, wakati walipokuwa akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliotaka kufahamu zaidi namna JKT linavyotekeleza jukumu la Malezi ya Vijana na umuhimu wake kwa Taifa.
Amefafanua kuwa nafasi zote zimepelekwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, hivyo amewataka wananchi kuepuka matapeli watakaotaka kiasi chochote cha fedha ili kuwapatia vijana wao nafasi hizo.

0 Maoni