NA REBECCA DUWE,Tanga
Mikakati thabiti ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii inahitaji ushirikiano wa makundi mbalimbali ya jamii nzima kwa ujumla ambapo Chama cha waandishi wa habari Wanawake Tanzania TAMWA imeazimia kutokomeza ukatili dhidi ya wananwake na watoto kupitia mradi wa Sauti zetu licha ya juhudi kubwa inayofanywa serikali nchini.
Mradi wa Sauti zetu unatekelezwa kwa ufadhili wa shirika la maendeleo la ujerumani GIZ ambao ndio unaoangazia kupunguza au kumaliza kabisa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa kutumia vyombo vya Habari,ambapo mradi huo unatekelzwa katika mikoa mitatu ambayo ni Daressalaam,Dodoma na Tanga.
Akitoa Tamko la Chama cha waandishi wa habari wananwake( TAMWA ) kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Chama hicho Dkt Rose Reuben ,meneja mikakati Sylivia Daulinge wakati wa mafunzo ya wadau,wanafunzi na waalimu yaliyofanyika jijini Tanga, alisema kuwa Tamwa imebaini kuwa bado kuna Ombwe kubwa la ukosefu Taarifa za matukio ya ukatili wa kijinsia katika jamii, kwamba waathrika kuogopa kutoa taarifa wanapofanyiwa Ukatili na ukosefu wa elimu wa Ukatili wa kijinsia.
Aidha alisema lengo la kukutana ni wadau hao ni kubadilishana uzoefu,kujifunza na kupata taarifa za hali ya ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Tanga lakini historia inaonyesha kuwa mkoa wa Tanga umeendelea kuwa kuwa eneo lenye kesi nyingi zaidi za matukio ya ukatili wa kijinsia.
Daulinge alieleza kuwa takwimu za mwaka 2023 kutoka ofisi ya Ustawi ya jamii mkoa wa Tanga zinaonyesha kuwa takribani asilimia 33 ya wanawake wamewahi kupitia ukatili wa kijinsia na kisaikolojia huku mwenendo huo ukionyesha kuongezeka kwa kasi didhi ya matukio hayo, lakini katika kanda ya kaskzini ,Tanga, Kilimanjaro na Arusha kesi ya ukatili wa kijinsia ni asilimia 83 jambo ambalo linionyesha kuwa ni mikoa yenye kesi nyingi zaidi za ukatili wa kijinsia.
Kaimu Afisa elimu shuleya msingi kutoka Lushoto mwalimi Beatusu Kiifumo alisema hali ya matukio ya ukatili kwa watoto imeendelea kuwemo katika Wilaya hiyo kwa baadhi ya wanafunzi kufelishwa kilazima ili asiendelee kusoma hali ambapo inakatisha ndoto za watoto hivyo ni vyema wa wazazi wakaona umuhimu watoto wao kusoma ili kutimiza ndoto zao.
Kwa upande wake Insepecta Grace Sandi Dawati la jinsia na watoto mkoa wa Tanga alieleza kuwa kwa mkoa wa Tanga matukio ya ukatili yameendelea kupungua kwa aslilimia 29 lakini pia utoaji wa taarifa pia umeongezeka kutokana na elimu inayoendelea kutolewa katika jamii.
Alisema watu wamekuwa wakiendelea kuripoti matukio ya ukatili ambapo watu wamepata mwaamko wa kutoa taari ya matukio ya ukatili kwa polisi kata, taarifa zimezidi kufichuliwa hususani kwa wanafunzi kipindi wanakuwa wanapofungua shule kumekuwa na taarifa za watoto wa kike kuozeshwa wakiwa katika umri mdogo na kupitia polisi kata wanapata taarifa kwa jamii kuendelea kupata elimu inayoedelea kutolewa.

0 Maoni