F WANANCHI WA KIJIJI CHA KIBAYA WATARAJIA KUPATA NEEMA BAADA YA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI HICHO KUKAMIKA MWESI WA TISA MWANZONI MWAKA HUU. | Muungwana BLOG

WANANCHI WA KIJIJI CHA KIBAYA WATARAJIA KUPATA NEEMA BAADA YA MRADI WA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI HICHO KUKAMIKA MWESI WA TISA MWANZONI MWAKA HUU.


 Na Rebecca Duwe TANGA


Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha Shilingi Milioni 45.7 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kibaya, iliyopo Wilayani Handeni, Mkoani Tanga.


Akizungumza wakat ziara yake ya kugua ujenzi wa mradi huo mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Rajab Abdalrahaman Abdalh alisema Ufadhili huo unalenga kuhakikisha miundombinu ya afya ambayo inamfikia mwananchi wa kawaida na kuondoa kero ya huduma za msingi vijijini.


Aidha alipotembelea mradi wa Ujenzi Wa zahanati hiyo aliweza kupata wasaa wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi ikiwemo ukosefu wa Maji ambapo alisema mh. Rais alitoa kiasi bilioni171 kwa ajili ya kero ya maji na changamoto ya Barabara Katika eneo la mkata wilayani humo.


Ziara yake hiyo imelenga kuimarisha Chama nabkujenga Chama cha Mapinduzi mkoani Tanga ambayo alianza Katika Wilaya Tanga mjini ,Pangani ,Mkinga Muheza,Lushoto Korogwe,Handeni ambapo Kesho atamalizia Wilaya Kipindi.


Aidha alisema wananchi wanapata kutiwa Moyo na viongozi wao pale ambapo wanakuwa na wazo la kuleta maendeleo Katika jamii ambayo yanafaa ya wananchi wote.


Amewaomba wananchi wote Katika maneno yote ya Mkoa wa Tanga kuanza wenyewe ili serikali iweze kuwashika mkono Kwa kuendeleza maendeleo kwa maslahi ya wote.


Samabmba na hayo mwenyekiti RAJABU amewaahidi wananchi wa kijij cha kibaya kuwa atahakikishi zahanati ya kijiji hicho walichokiomba wakati Ziara yake aliyofanya 2024 inakamilika iwe mvua ama iwe jua ,usiku au mchana ili kuwondolea wananchi adha ya kufuata Huduma za afya umbali mrefu ambayo inawa sababushia wakati mwingine wanawake kujifungulia njiani.


Alisema wakati huo alipokuwa anafanya Ziara yake Katika Wilaya hiyo alipofika Katika eneo alizuia na wananchi wa kijiji cha kibaya wilayani Handeni walizuia msafara wake nakufika Katika eneo hilo ambapo kuna eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho ambapo alitoa shilingi milioni 10.ili kuanza ujenzi wa mradi huo.


Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Handeni Steven Saitoti alisema serikali ya daktati Samia Suluhu Hassani imetoa shilingi milioni 45.7 kutoka serikalini Kwa ajili kuendeleza Ujenzi wa zahanati hiyo ambayo unatarajiwa kukamilika mwezi wa tisa mwanzo mwaka huu.


Naye Mkuu wa Wilaya Handeni Salum Nyamwese alisema kuwa wao kama Wilaya wanahakikisha jengo la zahanati hiyo inakamilika Kwa wakati ukiwa Kupitia michango mbalimbali ya wadau wa Chama cha Mapinduzi CCM na serikali ilia kufika hatua ya kuwondolea wananchi ada kufuata Huduma ya afya umbali mrefu.

Wakizungumza kwa hisia za shukrani, wananchi wa Kijiji cha Kibaya wameeleza kuwa kukamilika kwa zahanati hiyo ni ukombozi mkubwa.


Sambamba na hayo baadhi ya wananchi wa kijiji hiyo walimpongeza Rais Samia Suluhu Hassanina Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga Kwa kuweza kuwaunga mkono ili kuweza kuwaondoa kwenye changamoto ya Huduma za Afya kijijini hapo.


Mwanahawa Athumani ni miongoni mwa wanawake walitoa shukrani Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, ambapo alisema Kwa itakuwa ni furaha kuwa wao kama wamama kupata ukombozi Kwa kuwepo Kwa zahanati hiyo kwana walikuwa wanaogopa kuzaa Kwa sasa baadaya zahanati kukamilika watazaa bila wasiwasi.

 

Chapisha Maoni

0 Maoni