NA REBECCA DUWE TANGA
Hospitali ya Rufani KCMC ,imetangaza kuwa imeanza ujenzi wa Taasisi ya Moyo KCMC ili kusadia na kupunguza gharama inayotokana na safari ya umbali mrefu na foleni ya huduma kwa Wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI wakiwemo wale wanaosafirishwa nje ya Nchi .
Sambamba na wadau wa Maendeleo Mkoa wa Tanga wanatarajiwa kusaidia kuchangia kiasi cha Sh.Bil 3 kwaajili ya ununuzi wa vifaa kati ya Bil.25 zinazohitajika katika ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo mpaka sasa kiasi cha Sh.22 Bil kimeshapatikana kutoka kwa Wadau wa Maendeleo nje ya Nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt.Batilda Buriani, alisema ujenzi wa Taasisi hiyo unakwenda kuwasaidia wakazi wa Mikoa ya Kanda ya kaskazini Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuwapunguzia gharama kubwa wanayotumia ya kwenda katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI pamoja na kuokoa gharama kubwa,
"Ujenzi wa Taasisi hii ya magonjwa ya moyo utawasaidia wakazi wa Tanga na Mikoa ya Kanda ya kaskazini lakini pia hata watu wengine kutoka Mikoa mingine ya jirani, kwasasa Wagonjwa wa moyo wanalazimika kusafiri hadi jijini Dar e S salaam katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI lakini wengine wanapata rufani yakwenda nje ya Nchi, lakini ujio wa Taasisi hiyo utaongeza upana wa huduma za moyo Nchini na kupunguza idadi ya Wagonjwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI" Alisisitiza Dkt.Batilda
Dkt.Batilda alisema asilimia 60 ya Wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete JKCI wanatoka Kanda ya kaskazini na kuwataka wadau wa Maendeleo mkoani Tanga kujitokeza kwa wingi May 30 kwenye harambee na wadau wa Maendeleo ukumbi wa Tanga Beach resort ili kuchangia pamoja na kupea fursa za ujenzi wa Taasisi ya moyo KCMC,
"Niwaombe sana wadau wa Maendeleo Mkoa wa Tanga tujitokeze kwa wingi kwenye harambee maalumu ili tuweze kuchangia ujenzi wa Taasisi ya moyo KCMC,lakini pia kwa wale ambao hawatoweza kufika naomba tujitokeze kwa michango"Balozi Batilda
Kwa upande wake afisa miradi na mipango wa KCMC Emanuel Biyanchi alisema kuputia hafla hiyo wadau watapata taarifa sahihi kuhusu fursa kwenye sekta ya Afya uwekezaji,huduma za Afya miradi ya maendeleo na maeneo ya mashirikiano ya kibiashara na kijamii ndani KCMC na taasisi zake.
Aliongeza kusema kuwa sekta ya Afya si tu eneo huduma pekee bali ni fursa kwa wawekezaji , ajira,ubunifu na Tahiti na maendeleo ya jamii.
samabamba na hayo alisema hafla hiyo itatoa nafasi majadiliano yankaribu kati y wadau, wawekezaji Viongozi na Taasisi mbalimbali kuhusu namna bora ya kushirikiana kati ya miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma za Afya na ustawi wa jamii.

0 Maoni