TAKUKURU MKOA TANGA YAOKOA SH. 116.2KATIKA MIRADI YA ELIMU TANGA MJINI NA SH. 106.3 WILAYA YA MUHUEZA MKOANI TANGA.


Na Rebeca Duwe Tanga 

Taasisi ya kuzia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa Tanga imsema imfanikiwa kuokoa fedha kiasi sh.milini 116.2 na kusiadia kukamilika kwa baadhi ya miradi ya elimu iliyokuwa imekwama kutokana na changamota za kitendaji na ununuzi.


  Hayo aliysema Mkuu wa Taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Tanga Ramadhan Nduwata wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni taarifa ya miezi mitatu January hadi Mach mwaka huu ambapo alisema kuwa hayo mafanikio ni matokeo ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo. 

.

Alisem kuwa miongoni mwa miradi ambayo imenufaika ni ujezi wa madarasa mawaili na vyoo katika shule ya sekondari Chongeleani yenye thamani ya shi.milioni 93,mradi huo ulikwama kutokana na makadirio yasiyoendana na bei halisi ya soko hali iliyosababisha zabuni kushindwa kupatikana kupitia mfumo wa Nst.


Hata hivyo baada ya hatua za usimamizi na uwajibikaji kuchukuliwa ,utekelezaji umeanza na unaendelea vizuri. alisma Ndwata


Pia mradi mwingine ambao TAKUKURU imefuatilia ni mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya kwa Bastola wilayani muheza wenye gharama ya sh.106.3 ambapo TAKUKURU ilisaidia milango kupwa vanish, kurekebisha mikanda ya Gypsum na kununuliwa kwa vitanda 57 ambapo thamani yake ni jumla ya milioni22.4 pamoja na maboresho ya miundo mbinu ya shule.


Aidha TAKUKURU mkoa Tanga ilifuatilia jumla ya miradi 49cya maendeleo yenye thamani ya 506.7 ikiwa ni miradi ya maji ,Afya,elimu Barabara na Utawala.


sambamba na hayo TAKUKURU mkoa Tanga imewafikia wananchi wapatao 189,521 katika kipindi hiko ambalo njia zilizotumika kuwafikia ni pamoja na semina57 mikutano ya hadhara 28 uimarishwaji w clubs za wapinga rushwa ,Maonesho 10 na vipindi vya radio 37 jambo limeongeza uelewa mkubwa na kukuza ushikiano wa wadau katika uzimuiaji wa rushwa.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi