Na Rebeca Duwe Tanga
Viongozi wa Dini wametakiwa kushirikiana na Jamii kwa kuzingatia suala la malezi ya watoto na vijana ili kuweza kupata kizazi kilicho bora katika jamii kwa maslahi mapana ya taifa kwa ujumla.
Haya aliyasema mwanyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga ustdh Rajabu Abdrahman wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Pangani katika kijiji cha Stahabu Pwani wakati dua ya kuombea dua ya kuwaombe ndugu waliotangualia mbele ya haki, ambapo alisema Suala la malezi na makuzi ya watoto ni jukumu la jamii kuweza kushirikia na viongozi wa dini ili kupata jamii ambayo ina msimamo mzuri wa kiimani na kimaadili.
Aidha Mwenyekiti Rajabu alisema kwamba ni vyema kushirikiana na viongozi wa Dini ili waweze kukemea mmomnyoko wa maadlii uliokitithiri katika Jamii kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza wimbi la wahalifu na kuwa na jamii salama.
"Viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuijenga jamii salama kwa kuwa wao ndio wanakaa na watu kwenye nyumba za ibada hivyo tukashirikana nao wote kujenga kizazi kijacho kwa kuweza kuwakemea maadili mabovu ili tuwe na kizazi kijacho "
alisema Mwenyekiti Rajabu.
Hata hivyo Mwenyekiti Rajab alisisitiza umuhimu wa malezi bora katika jamii hasa viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kukemea uovu kwa sababu ndio nguvu kazi ya baadaye na viongozi wa baadaye kwa aajili ya jami ijayao.
Kwa upande wake Mkuu Balozi Batilda Burian alimpongeza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga kwa kufanya jambo la kuwaunganisha viongozi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa na nje ya mkoa kwa ajili dua ya kuwombea ndugu waliotangulia mbele ya haki.

0 Maoni